Babati na mipango mingi mizuri isiyotekelezwa kwa muda,wafanyabiashara walia.
Wafanyabiashara katika soko NHC Babati wapo katika hatari ya kupata magonjwa ya mlipuko kutokana na uchafu uliorundikana eneo hilo na kukosa choo.
Wafanyabiasahara hao wameiomba serikali ya Hamashauri ya mji wa Babati kuwatatulia suala hilo kwa haraka ili kunusuru afya zao.
Wameeleza kuwa kutokana na dampo hilo inakuwa vigumu hata biashara yao kwenda kutokana na wateja kushindwa kufika maeneo hayo kwa harufu mbaya inayotoka katika Dampo hilo. 
Wameeleza hayo wakati walipotembelewa sokoni hapo hivi karibuni na kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi ya mji wa Babati iliyokuwa ikikagua miradi mbali mbali inayotekelezwa kwa ilani ya chama hicho inayosimamiwa na Rais John pombe Magufuli. 
Katika ziara hiyo kamati iliweza kubaini udhaifu mkubwa katika utekelezaji wa miradi hiyo ikiwemo kuchelewa kukamilika kwa muda ujenzi wa madarasa katika shule ya msingi Nangara na moja shule ya sekondari Nangara, majengo yaliyodumu kwa zaidi ya miaka 5 bila kukamilika.
Kwa upande wake kaimu mkurugenzi wa mji wa Babati Nuagi Karengi ameihakikishia kamati kuwa mpaka march 2017 ujenzi huo utakuwa umekamilika..
Naye Eng. Salvatory Yambi amesema kuwa kwa sasa Halmashauri ya mji wa Babati inaendelea na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bara bara ya Babati hadi katika kijiji cha Nakwa kwa kiwango cha moram urefu wa Km 4.5 itakayogharimu shilingi milioni 51,845,000.
Diwani wa kata ya Mutuka mheshimiwa Yona Hadwe Wao, amesema kuwa anasikitishwa na ofisi ya mkurugenzi kushindwa kutatua changamoto za bara bara ya mutuka ambayo ndio kiunganishi cha Babati.
Kaimu mkurugenzi amesema kuwa Halmashauri imetenga shilingi milioni 21 kwa ajili ya ukarabati wa bara bara hiyo inayopitia chuo cha ufundi Veta.
Halmashauri ya mji wa Babati imetenga shilingi million 48,38,723 kwa ajili ya kuboresha mnada wa gendi kwa kuzungusha uzio katika eneo lote ili kuziba mianya ya watu kukwepa kulipa kodi pamoja,kujenga choo cha pili,miundo mbinu ya maji pamoja na kujenga karo kwa ajili ya kuchinjia.
Kamati hiyo ya siasa ya chama cha mapinduzi Ccm Babati ikiongozwa na Mwenyekiti wake na katibu Bernad Ghati wakiwa wameongozana na wataalamu kutoka serikali ya Halmashauri ya mji wa Babati, ilitembela hospitali ya mji wa Babati Mrara katika hodi ya wazazi ambapo watoa huduma katika hodi hiyo wameiomba serikali ya iongeze jengo la hodi hiyo kwani ni ndogo hali inayowalazimu kulala wawili wawili kwa kuwa hakuna pa kuweka vitanda,upungufu wa vifaa vya upasuaji na matundu ya vyoo.
Pia kamati hiyo ya siasa ya chama cha Mapinduzi iliweza kufika katika kituo cha afya kata ya Bonga na kukuta changamoto ya gari la wagonjwa,Chumba cha kuhifadhia maiti huku uongozi ukidai kuwa gari
lipo gereji kwa matengenezo tangu mwaka 2010 na inahitajika shilingi milioni 7 kukarabatiwa.
Katika ziara hiyo ya kukagua miradi inayotekelezwa na chama tawala,eneo la madawati tu ndio lililokamilika kwa asilimia 100% katika shule zote kamati ilizozikagua huku mradi wa bara bara ya lami ukiwa katika hatua za mwisho.

No comments: