Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na utashughulikiwa – Nape
Ukinunua CD isiyo na stika, wewe ni mwizi kama wezi wengine na utashughulikiwa – Nape
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye baada ya
kufanya ziara Ijumaa hii katika maeneo ya Kariakoo kukagua na kukamata
CD ambazo hazina stika ya TRA, amewataka watanzania kuacha tabia ya
kukunua CD ambazo hazina stika za TRA.
Nape akitoa CD fake madukani
Akiongea na waandishi wa Habari katika msako huyo, Nape amesema
yeyote anayekamatwa na CD ambao haina stika ya TRA atashtakiwa kwa kosa
la kuhujumu uchumi.“Kila anayenunua sasa kazi ya sanaa ambayo haina stika ya TRA naye ni mwizi kwa kama mwizi yoyote sababu ameshirikiana na muuzaji ambaye hajalipa kodi, hata tukikukuta na CD moja haina stika wewe ni mwizi kama mwizi mwingine tutashughulika na wewe,” alisema Nape.
Katika ziara hiyo zaidia ya maduka 40 yamefungwa huku CD fake zikichukuliwa kwa ajili ya kuaribiwa.
No comments: