Home Ads


Waziri wa ujenzi na mawasiliano Awataka wakandarasi wakamilishe BaraBara kwa wakati wananchi wanateseka

Waziri wa ujenzi,mawasiliano na uchukuzi Profesa Makame Mbarawa
WAZIRI wa ujenzi, mawasiliano na uchukuzi Makame Mbarawa,amemtaka mkandarasi China Railways Seventh Group Co.L.tdanaejenga barabara Kwa kiwango cha lami kutoka Bonga-Mela yenye urefu wa km 88.8 kwa gharama ya  Tshs Bil 83, kuhakikisha wanakamilisha kwa haraka barabara hiyo na kwa muda uliopangwa ili kuwapatia unafuu katika usafiri Wananchi wa mikoa ya Dodoma na Manyara.
Mradi huo wa barabara unajengwa kwa ufadhili wa serikali,benki ya maendeleo ya Africa(ADB),na Shirika la maendeleo ya Japan(JIKA) kwa gharama ya Tsh bil.83  ambapo waziri alisema  Serikali itahakikisha inalipa fedha zao kutokana na vyeti vyao watakavyopeleka waweze wajiridhisha ili kazi yao isiweze kusimama kwani kusimama kwa kazi itasababisha kuchukua muda mrefu wa kumalizika kwa mradi huo.
Waziri Mbarawa aliyasema hayo jana wakati wa ziara yake ya kukagua mradi wa Barabara wa kiwango cha lami wenye km.88.8 kutoka Bonga-Mela mkoani Dodoma unaoendelea kujengwa,ambapo akiwa kolo wilayani kondoa mkoani Dodoma alimtaka msimamizi wa Barabara hiyo ambaye ni mhandisi mkazi Kini Kuyonza kuhakikisha Barabara hiyo inajengwa kwa viwango kwani fedha zinazotumika kuwalipa ni  nguvu za watanzania za walipa  kodi.
“Kama Barabara hiii itajengwa kwa miaka kumi na tano na yenyewe inatakiwa idumu kwa miaka hiyo lakini sio barabara inajengwa kwa miaka kumi na tano halafu ndani ya miaka miwili inabomoka ,fanya kazi kwa wako mzuri na kama serikali itafanya wajibu wake kwa kuwalipa kutokana na kazi yenu mtakayofanya”alisema Mbarawa.
Akijibu baadhi ya changamoto zilizotajwa na Mhandisi mkazi Kini Kuyonza  kuhusiana na Changamoto zinawakabili katika utekelezaji wa mradi huo ikiwemo kukosekana kwa ulinzi na usalama,fidia kwa Wananchi inayochangia ucheleweshaji wa utekelezaji wa mradi huo,Mbarawa alisema kwa upande wa ulinzi na usalama ni wajibu kwa Serikali kupitia Jeshi la polisi kulinda mali ya watanzania wote,Hivyowatashirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha Mkandarasi pamoja na Wananchi wanakuwa katika hali ya usalama na wanafanya kazi zao kwa usalama na utulivu.
Kwa upande wa fidia kwa Wananchi,waziri Mbarawa alisema kwamba ucheleweshaji wa fidia kwa Wananchi kunachangia kuchelewesha kazi ,hivyo kwa uapnde wa Serikali imekwisha lipa fidia japo kumekuwepo kwa mvutano na TANROAD na kuhakikisha kwamba endapo mvutano huo utaendelea kwa upande wa TANROAD,Serikali itafanya maamuzi sahihi ya kuhakikisha Wananchi wanaodai fidia wanalipwa.
“Hawezekani mtu mmoja anakaa kwenye kinyumba chake na anachelewesha mradi kwa miaka miwili kwa ajali hajalipwa fidia,tupo hapa kwa ajili ya kuwalinda watanzania wote ninaimani suala la fidia tutalimaliza na yale maeneo mnayodai mtaendelea nayo kufanya kazi vizuri”alisema waziri  
Hata hivyo aliitaka kampuni hiyo kushirikiana na meneja wa mikoa ya Manyara na Dodoma katika kutatua changamoto zinazowakabili mradi huo wa barabara ambazo zitaweza kufuatuliwa kwa pamoja  na kutafutiwa ufumbuzi wa haraka.

No comments:

Powered by Blogger.