Home Ads


Anna Makinda ataka mabadiliko ya sheria ya ndoa

Spika mstaafu wa Bunge, Anne Makinda, ameeleza kusikitishwa na kitendo cha serikali kushindwa kufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vilivyopo katika sheria ya ndoa ya mwaka 71 licha ya mchakato kuanza muda mrefu hali inayosababisha vitendo vya ukatili kuendelea.

Makinda ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, kwenye kongamano la kwanza kitaifa kutetea na kusimamia haki za wanawake kwa kuwawezesha na kusimamia kiuchumi ambapo amesema baadhi ya vipengele vilivyopo kwenye sheria ya ndoa inayotumika sasa vinakiuka na kukandamiza haki za wanawake hasa wale wasio na uelewa wa kisheria.
“Ningeomba serikali isaidie kufinance kucontribute kwasababu development partners kweli wanatusaidia watafika siku nyingine wataondoka. Tumemaliza si wanawapaga muda mradi wa miaka miwili mitatu subject to renew au basi kabisa, wanakuja viongozi wa nchi yanakuwa majitu wanasema hayo mambo out tutaweza kweli,” alisema.
“Sheria ya ndoa ya mwaka 71 inachelewa wapi? Tumeiimba wee toka mi nikiwa waziri mpaka leo kuna tatizo gani ile si iliandikwa na watu tu?,” alihoji
Liunge na KAMUTU  DIGITAL kwa habari zaidi



No comments:

Powered by Blogger.