Clinton azidi kuongoza katika uchunguzi wa maoni
Mdemokrat Hillary Clinton akiwa na uhakika wa ushindi katika uchaguzi wa rais wa Marekani mwezi ujao kwa sasa ameacha kumshambulia Trump na kuelekeza juhudi mpya ya kusaidia kuwachagua wademokrat wengi zaidi katika bunge kuu la Marekani ili kuweza kupata uungaji mkono anaohitaji kuweza kupitisha agenda yake.
Clinton alisema kwamba hafikiri tena kujibu uchokozi unaotolewa na Trump kwamba yeye ni fisadi na hafai kuingia White house.
Waziri huyo wa zamani wa mambo ya nje ambaye anatarajia kuwa rais wa kwanza mwanamke wa Marekani , aliwaambia waandishi wa habari akiwa kwenye ndege yake ya kampeni Jumamosi katika siku 16 za mwisho kabla ya uchaguzi wa Novemba 8 kuwa anapanga kusisitiza umuhimu wa kuwachagua wademokrat kwenye mabaraza ya wawakilishi na Senet katika juhudi ya kuchukua tena udhibiti wa mabaraza hayo ambayo yanashikiliwa na warepublikan .
Clinton ambaye anaongoza kwa kati ya asili mia 9 hadi 10 katika uchunguzi wa maoni wa kitaifa ameamua kupelekea mamilioni ya dola kutoka kampeni yake na kuingiza katika kampeni za wabunge wa majimbo ambayo kwa kawaida huwapigia kura warepublikan katika juhudi ya kuongeza uongozi wake dhidi ya Trump na kuwasaidia wagombea wademokrat wanaogombea dhidi ya warepublikan wanaoshikilia majimbo hayo.
Wachambuzi wanasema wademokrat huenda wakachukua tena udhibiti wa baraza la senet , lakini wana kazi kubwa katika baraza la wawakilishi ambapo warepublikan wanadhibiti kwa karibu ya viti 30.
fualia ; kdigital48.blogspot.com
No comments: