Home Ads


EMPIRE;Huenda AKA akapata shavu kwenye tamthilia ya Empire msijao

mu uHuenda AKA akapata shavu kwenye tamthilia ya Empire msijao


Huenda rapper AKA wa Afrika Kusini akapata shavu kwenye tamthilia ya Empire msimu ujao.
13380822_1588006504863379_623846437_n (1)
Waigizaji wa show hiyo iliyotokea kupendwa duniani, Taraji P Henson (Cookie) na Terrance Howard (Lucious Lyon) wapo Afrika Kusini katika ziara maalum iliyoandaliwa na kampuni ya Multi Choice.
AKA aliungana na mastaa hao katika moja ya hafla ya kukutana na kusalimiana na mashabiki wa Afrika Kusini ambapo pia alitumbuiza. Rapper huyo aliyefanya kazi na Diamond na Joh Makini alishare video ikimuonesha akiongea na mastaa hao na kuwaeleza kuwa angependa pia kuigiza kwenye tamthilia ya Empire.
Terrence anasikika akimueleza kuwa wataongeza na muongozaji, Lee Daniels ili amuongeze.
“Lucious & Cookie enjoyed the show. Maybe they’ll give me a role on Empire. Tell Lee Daniels about the design,” aliandika AKA kwenye video hiyo na kumtag Lee Daniels.
Taraji aliirepost video na kuandika: You were a wonderful host @akaworldwide I AM A BIG FAN OF #AfricanMusic

No comments:

Powered by Blogger.