Magufuli kuhamia Dodoma?
RAIS John Magufuli ameonesha nia ya kuhamia Dodoma kwa kuanza kushughulikia masuala muhimu, ikiwamo ya kuzindua awamu ya kwanza ya upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma na kuhamishia maadhimisho ya Siku ya Mashujaa mkoani Dodoma.
Akizungumza juzi wakati wa mkutano wa kitaifa wa amani ulioandaliwa na Jumuiya ya Ahamadiyya, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema katika kuonesha dhamira ya kuhamia Dodoma ambao ulitangazwa kuwa Makao Makuu ya Tanzania miaka ya 1970, Rais alielekeza fedha zilizobaki kwenye bajeti iliyopita zitumike kwa ajili ya upanuzi wa uwanja wa ndege ambao pia ujenzi wake utazinduliwa na Rais mwenyewe Julai 22, mwaka huu.
Mh. Rugimbana amesema Rais Magufuli pia ameagiza maadhimisho ya Siku ya Mashujaa mwaka huu yahamie Dodoma ambapo kwa miaka mingi sasa yamekuwa ikifanyika kwenye Viwanja vya Mashujaa, Mnazi Mmoja Dar es Salaam.
No comments: